
Front view of Kenyatta University Teaching, Referral and Research Hospital.
UPASUAJI WA UJENZI UPYA WA MATITI WAZIDI KUPATA UMAARUFU
WANAWAKE WENGI WA KENYA WANAZIDI KUFUATA UPASUAJI WA UJENZI UPYA WA MATITI BAADA YA KUYATOA KUTOKANA NA SARATANI.
KULINGANA NA DKT. JOHN-PAUL OGALO, DAKTARI WA UPASUAJI KATIKA HOSPITALI YA MAFUNZO, UTAFITI NA RUFAA YA CHUO KIKUU CHA KENYATTA (KUTRRH), TAYARI WAGONJWA 50 WAMEFANYIWA UPASUAJI HUU TANGU ULIPOANZISHWA MWAKA WA 2021.
DKT. OGALO ALIZUNGUMZA WAKATI WA KONGAMANO LA PILI KUHUSU UJENZI UPYA WA MATITI NA UREMBO LILILOFANYIKA KUTRRH, LIKIHUDHURIWA NA WATAALAMU KUTOKA KOTE DUNIANI.
KONGAMANO HILO LILIWALETA PAMOJA MADAKTARI KUTOKA AFRIKA, ULAYA NA AMERIKA KUBADILISHANA UZOEFU NA MAARIFA KUHUSU MATIBABU YA SARATANI YA MATITI NA UPASUAJI WA UJENZI UPYA UNAOFUATIA.
DKT. ANTHONY KAMAU, KAIMU MKURUGENZI WA HUDUMA ZA KLINIKI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA KU, ALISEMA KUWA AWALI UPASUAJI HUU HAUKUFADHILIWA NA SHA NA AKATOA WITO KWA WANAWAKE WENGI ZAIDI KUJITOKEZA KUFANYIWA UTARATIBU HUU.
DKT. NANCY VAN LAEKEN KUTOKA KANADA ALISEMA KUWA HAKIKISHO BORA ZAIDI LA KUISHI BAADA YA SARATANI NI UTAMBUZI WA MAPEMA NA MATIBABU, AKISISITIZA KUWA HAKUNA UHAKIKA KWAMBA NCHI ZILIZOENDELEA ZINA ASILIMIA KUBWA ZAIDI YA WAATHIRIWA WANAOPONA.
MWISHO